Thursday, 24 November 2016

NIPE TENA





kukivunja si hoja unipacho naridhika
sichelei kungoja, mwenzio nataka
nipe japo kimoja, cha ubeche nataka
nipe tena na leo, kabla kesho kufika.

eti pako pakavu vipi mchuzi wataka?
kilaini ntie nyavu, hata futa ntapaka
si haja kutia kovu, maridadi ntakata
nipe tena na leo, kabla kesho kufika.

nipe pia na leo, tena zaidi ya jana
nipe vya leo leo, nnahamu tena sana
nipe kw msusio, msuso wa mana
nipe tena na leo, kabla kesho kufika.

nipe tena ntambe, ladha ya kachumbari
tena pale kwa pembe, na viungo mbambali
nipe nijirambe, nipe usibakhili
nipe tena na leo, kabla kesho kufika.

haki ukatavyo, ikata bakuli
navye unyonyavyo, mi mwenzo si hali
navye nlambavyo, chumvi haikithiri
nipe tena leo, kabla kesho kufika.

eti bebi yalaa, na sauti matata
mara bebi aa, vipi imepita?
no.. bebi aa, nini sijui tata
nipe tena na leo, kabla kesho kufika.


No comments:

Post a Comment